Siku ya Wakunga duniani kitaifa kufanyika Simiyu
Maadhimisho ya Siku ya Wakunga duniani kitaifa mwaka huu yanatarajiwa kufanyika kesho Jumapili Mei 5, mkoani Simiyu, ambapo mgeni rasmi atakuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndungulile.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumamosi na Mkuu wa mkoa wa huo, Anthony Mtaka, Naibu Waziri huyo atamwakilisha Makamu wa Rais wa Samia Suluhu Hassan.
Mtaka amesema kuwa maandalizi yote ya maadhimisho hayo yamekamilika kwa asilimia 100, ikiwamo wakunga kutoka katika mikoa mbalimbali wakiongozwa na viongozi wa chama chao (TAMA) kuwasili mkoani humo.